Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Arumeru ikiongozwa na Mwenyekiti wake Bw Jerry Murro imewakamata watu 7 wakiwemo wenyeviti wawili wa vitongoji wakiwa na vifaa vya ujenzi zikiwemo nondo wanazodaiwa kuiba kwenye mradi wa maji unaotekelezwa kwenye eneo hilo kwa gharama ya shilingi bilioni 520.
Jeshi la Polisi limethibitisha kukamatwa kwa watu hao ambao baada ya kuhojiwa wameelezea namna walivyoshiriki katika wizi huo.
Uchunguzi wa kuubaini mtandao huo wa wizi wa vifaa vya ujenzi katika miradi mbalimbali inayotekelezwa kwa fedha za serikali unaendelea ikiwa ni pamoja na kubaini wanunuzi wa bidhaa hizo.
