
Shirika la afya duniani (WHO ) linatoa wito kwa watu kuahirisha safari zao za likizo na baadhi ya matukio ya msimu wa sikukuu ili kusaidia kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona, wakati huu ambao kirusi kipya cha Omicron kinaendelea kusambaa kwa kasi duniani.
Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani Tedros Ghebreyesus amesema kufutwa kwa baadhi ya matukio yaliyopangwa ni bora, kuliko kuondoa uhai na kuongeza kuwa maamuzi magumu ni lazima yakachukuliwa.
