Back to top

Wizara ya afya yaagiza Halmashauri kutunga sheria kudhibiti ombaomba.

28 February 2020
Share

Wizara ya Afya Maendeleo ya jamii Jinsia Wazee na Watoto imeziagiza Halmashauri zote za majiji kutunga sheria kama walivyofanya Halmashauri ya Ilala kuwachulia hatua kali wale wote watakaokuwa wakiwasaidia ombaomba katika maeneo mbalimbali sambamba na kuwaweka ndani wazazi wanaowatumia watoto hao kufanya hivyo.


Hayo yamesemwa na  Naibu waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii jinsi Wazee na Watoto Mh Dk Faustine Ndugulile wakati akizungumza na  Taasisi ya SOS inayojisughulisha na malenzi ya vijana.