Back to top

ZAIDI YA BILIONI 4 KUTATUA SHIDA YA MAJI KARATU

02 August 2022
Share

Waziri wa Maji, Mhe.Jumaa Aweso amesema serikali inakusudia kutoa Shilingi Bilioni nne na nusu kwa ajili ya kuondoa shida ya upatikanaji wa maji kwa wananchi wa Wilaya ya Karatu.

Amesema hayo wakati wa kikao chake na Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo ya Karatu pamoja na viongozi wa dini na wataalam wanaounda kama ti iliyundwa kuchunguza gharama za maji.

Katika kikao hicho Waziri Aweso ameagiza kuundwa kwa chombo kimoja kitakachosimamia huduma ya maji.

Akitoa taariifa ya kamati iliyoundwa kufanya tathmini ya hali ya upatikanaji wa maji katika Wilaya hiyo, Mwenyekiti wa kamati, Bwana Jacob Kingaziamesema uwepo wa chombo zaidi ya kimoja umechangia tatizo.