Back to top

Zaidi ya wa watu 1,018 wafariki kutokana na virusi vya Corona.

11 February 2020
Share

Timu ya wataalamu wa Shirika la Afya duniani imeelekea Beijing nchini China kuchunguza mlipuko wa virusi vya Corona, hadi sasa virusi hivyo vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 1,018 wengine zaidi ya 43,104 wakiambukizwa, huku waliopona ikielezwa wamefikia 4,043.

Jana Rais wa China, Xi Jinping aliwatembelea wagonjwa wa virusi vya Corona pamoja na maafisa wa afya ambao wanawahudumia wagonjwa hao ambapo alionekana amevalia kitambaa cha kufunika uso kwa ajili ya kujikinga na pia alipima afya yake.

Rais Xi amemteua Waziri Mkuu Li Keqiang kuongoza kundi la wafanyakazi litakaloshughulikia mlipuko wa virusi hivyo na mwezi uliopita Li aliutembelea mji wa Wuhan ambako virusi hivyo vilianzia.

Aidha Rais Xi Jinping ameviita virusi vya Corona kama 'Janga', Xi amesema hatua kali zaidi zitachukuliwa kwa ajili ya kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo.