Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameondoka nchini kuelekea Cairo nchini Misri kwa Ziara ya Kiserikali ya siku tatu.
Ziara hiyo ya Kiserikali inafuatia mwaliko wa Rais wa Misri, Mhe. Abdel Fattah Al Sisi.
Katika ziara hiyo, Mhe. Rais Samia pamoja na mambo mengine anatarajiwa kufanya mazungumzo na mwenyeji wake katioa maeneo kadhaa ya ushirikiano kati ya Tanzania na Misri ikiwemo nyanja za diplomasia, uchumi, siasa, utalii na huduma za kijamii.
Aidha Mhe. Rais Samia na mwenyeji wake Mhe. Rais Abdel kwa pamoja wanatarajiwa kushuhudia utiaji saini mkataba mmoja (1) na hati saba (7) za makubaliano kati ya Tanznaia na Misri.
