
Mfalme Charles III wa Uingereza amegundulika kuwa na saratani, ambapo kutokana na hali hiyo, Mfalme huyo atasitisha majukumu yake kwa umma, ili apate matibabu.
.
Taarifa hiyo imetolewa na Kasri la Buckingham, ingawa haijabainisha kuwa Saratani hiyo ni ya nini, lakini imesema kuwa si ya tezi dume, lakini imegunduliwa hivi karibuni wakati akipatiwa matibabu ya uvimbe katika tezi dume.
.
Mfalme, mwenye umri wa miaka 75, licha ya kusitisha majukumu yake kwa umma lakini ataendelea na jukumu lake la kikatiba kama mkuu wa nchi.
