Back to top

WAWAKILISHI BUNGE LA MAREKANI WATETA NA WAZIRI KAIRUKI.

02 June 2024
Share

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki, amekutana na kuzungumza na ujumbe wa Wawakilishi 11 wa Bunge   kutoka nchini Marekani, ambao wamekuja nchini Tanzania, kujifunza kuhusu masuala mbalimbali ya Uhifadhi.

Waziri Kairuki amesema wamezungumzia  kuhusu masuala mbalimbali ya uhifadhi, urejeshaji wa nyara, kudhibiti  ujangili na kushirikiana katika kuelimisha wananchi masuala ya uhifadhi na mipaka yao. 

Akizungumza kwa niaba ya Wawakilishi hao, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maliasili kutoka Marekani, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Arkansas, Mhe. Bruce Westernman, amesema kuwa wamepata fursa ya kujifunza kuhusu uhifadhi na  kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.