
Mshambuliaji mpya wa Azam FC, Donald Ngoma,ameondoka kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya.
Ngoma ambaye ni raia wa Zimbambwe, aliyesajiliwa na Azam kutoka Yanga,amesafirishwa kuelekea jiji la Cape Town ili kupata vipimo vya afya ili kuona tatizo lipi linalomsumbua na kushindwa kucheza takribani msimu mzima wa 2017/18 kutokana na kusumbuliwa na majeruhi.
Ofisa wa Habari wa Azam FC, Jaffar Maganga, amesema kuwa watakuwa tayari kumgharamikia Ngoma endapo itabainika ana tatizo katika afya yake na kama atakuwa yuko sawa atarejea nyumbani.