Jeshi la polisi mkoani Arusha linawashikilia watu wanne wanaohusishwa na mtandao wa kimataifa wa kutengeneza noti bandia ambao wamekamatwa wakiwa na maelfu ya noti bandia za nchi zaidi ya 12 zikiwemo dola za Kimarekani , Euro na fedha nyingine.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha Bw Ramadhani Ng'anzi amesema watuhumiwa hao wanaoendelea kuhojiwa pia wamekutwa na mashine na baadhi ya vifaa vya kutengeneza fedha hizo bandia wakiwa wameshatengeneza kiasi kikubwa cha fedha za nchi mbalimbali .