Back to top

Wahamiaji zaidi ya mia tano na mawakala wao wakamatwa Pwani.

04 February 2019
Share

Idara ya uhamiaji mkoa wa Pwani imekamata wahamiaji zaidi ya mia tano  na mawakala wao katika operesheni iliyofanyika wilayani Bagamoyo na maeneo mengine kati ya Januari mosi hadi sasa.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kibaha Afisa uhamiaji mkoa wa Pwani Kamishna mwandamizi msaidizi wa idara ya  uhamiaji Bw.Abdallah Towo amesema operesheni hiyo ilienda sambamba na udhibiti wa njia za panya na ukaguzi vibali vya wageni wanaoishi na kufanya kazi nchini .

Aidha Bw.Towo amesema katika idadi hiyo baadhi yao wamerudhishwa nchini kwao na wengine kufikishwa mahakamani.