Back to top

Waziri Mkuu amsimamisha kazi mweka hazina Kibondo.

19 February 2019
Share

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi mweka hazina wa Halmashauri ya wilaya ya Kibondo, Thomas Chogolo ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili za ubadhilifu wa makusanyo ya mapato ya halmashauri hiyo.

Mh. Majaliwa  amewataka watendaji wa halmashauri huyo kumaliza haraka migogoro yao ya kiutendaji kabla ya Serikali haijawachukulia hatua kwani wanachokifanya ni kinyume na maelekezo yake.

Amechukua hatua hiyo wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo.

“Katika Serikali hii suala la ukusanyaji wa mapato ni jambo nyeti na limepewa kipaumbele, hivyo ni lazima fedha inayokusanywa itumike kama ilivyokusudiwa ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi.”Amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

Waziri Mkuu ameongeza kuwa  wananchi wa halmashauri hiyo wanalipa kodi kupitia kwa watendaji wa kata katika maeneo yao lakini  mweka hazina haingizi kwenye mfumo wa Serikali.