Back to top

Andreescu amhenyesha mkongwe wa tenisi Serena Williams.

09 September 2019
Share

Mwishoni mwa wiki hii imekuwa mbaya kwa mcheza tenisi bora wa kike Serena Williams baada ya kukubali kuangushwa na mchezaji mdogo katika fani ya tenisi toka Canada, Bianca Andreescu.

Andreescu amekuwa raia wa kwanza wa Canada kutwaa ubingwa wa michuano mikubwa ya tenisi ya US Open baada ya kupata ushindi wa seti mbili za 6-3, 7-5.

Andreescu mwenye umri wa miaka 19 amekuwa mchezaji wa kwanza kutwaa taji hilo la ubingwa wa Grand Slam.

Serena mwenye umri wa miaka 37 amepata pigo la pili mfululizo katika fainali za Grand Slam katika michuano hiyo iliyofanyika Flushing Meadows, baada ya mwaka jana kushindwa na Naomi Osaka.