
David De Gea na Paul Pogba hawatokuwemo kwenye kikosi cha Manchester United dhidi ya Liverpool jumapili hii.
Manchester United watawakaribisha Liverpool ambao wameshinda michezo yao yote ya ligi hadi sasa huku kikosi cha United kikiwa katika nafasi mbaya kwa point chache walizojikusanyia.
Habari mbaya kwa United ni kwamba watawakosa wachezaji wao wawili Pogba na golikipa De Gea katika mchezo huo.
De Gea amefanyiwa vipimo Jumanne ya jana baada ya kuumia akiwa katika majukumu ya timu ya taifa ya Hispania kuwania kufuzu michuano ya Euro 2020 dhidi ya Aweden na hivyo hatokuwa vizuri kiafya katika mechi hiyo ya jumapili.
Kwa upande wake Paul Pogba naye ambaye alikuwa Dubai katika kipindi hiki cha mapumziko ya kupisha kalenda ya FIFA bado hajawa vizuri kiafya kiasi cha kucheza mchezo huo.