Back to top

Wachina 100 wanaswa wakichimba dhahabu kinyemela Geita.

22 October 2019
Share

Kamati ya Ulinzi na Usalama, Mkoa wa Geita imewakamata raia 100 kutoka China wakituhumiwa kuendesha shughuli za uchimbaji wa dhahabu  kinyemela katika mgodi wa dhahabu wa Eagle Brand uliopo Kata ya Magenge Mkoani Geita.

Operesheni hiyo iliongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi ya Mkoa  wa Geita, Mhandishi Robert Gabriel amesema watapita kwenye migodi yote usiku na mchana ili kuwakamata wageni wanaofanya kazi kinyemela.

Afisa Kazi Mkoa wa Geita, Bw.Mohamedi Majaliwa amesema wageni walioingia nchini kinyume na sheria watalipa faini Shilingi Milioni kumi pamoja na kifungo cha miaka miwili jela kwa kukiuka sheria ya ajira.

Msimamizi wa mgodi huo, ambaye ni raia wa kigeni amekiri kuwa na wafanyakazi hao bila kibali akieleza kuwa utaratibu wa kutafuta vibali unaendelea.