
Ushindi wa mabao 9-0 ugenini dhidi ya Southampton usiku wa kuamkia leo umeifanya timu ya Leicester City kuvunja rekodi ya ushindi wa mabao mengi ugenini kwenye ligi ya England iliyowekwa na Manchester United tarehe 06 Februari 1999 kwa kuifunga Nottingham Forest mabao 8-1.
Lakini kabla ya hapo Nottingham Forest nao walishaishikilia rekodi hiyo ya kufunga mabao mengi ikiwa ugenini baada ya kufanya hivyo dhidi ya Sheff Weds kwa kuifunga mabao 7-1 mnamo tarehe 01 April 1995.
Na sasa Leicester City ndio wanashikilia rekodi hiyo ya kushinda mabao mengi ugenini kwenye ligi ya England ikiwa ni baada ya miaka 20 kupita.
Lakini katika rekodi ya timu iliyoshinda mabao mengi zaidi ikiwa nyumbani bado Manchester United inashikilia rekodi hiyo baada ya kuifunga mabao 9-0 timu ya Ipswich na hiyo ilikuwa ni tarehe 04 March 1995.