Back to top

Wanafunzi 350 sekondari ya Marumba Tunduru hawajulikani walipo

27 October 2019
Share

Wanafunzi 350 wa shule ya sekondari ya Marumba katika wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma ambao walipaswa kuwepo shuleni hapo hawajulikani walipo huku mwalimu mkuu wa shule hiyo, Bw. Michael Kapinga akisema tatizo kubwa ni mwamko mdogo wa elimu kwa wazazi hali ambayo inachangia utoro uliokithiri kwa wanafunzi na wengine kupata ujauzito.
 

Bw.Issa Sinambi ni afisa elimu kata ya Marumba wilaya ya Tunduru anasema shule hiyo inategemewa na wanafunzi wa kata mbili na kwamba tatizo kubwa linalochangia utoro huo ni baadhi yao kukaa umbali mrefu.