Back to top

Messi kurejea kikosini baada ya kumaliza kifungo.

28 October 2019
Share

Mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi anatarajia kurejea tena kwenye timu yake ya taifa ya Argentina katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Brazil utakaopigwa tarehe 15 mwezi Novemba nchini Saudi Arabia na dhidi ya Uruguay tarehe 19 Novemba nchini Israel baada ya kumaliza kifungo chake cha miezi mitatu.


Messi alifungiwa miezi mitatu kuitumikia timu yake ya taifa na shirikisho la soka la Amerika Kusini 'South American Football Confederation' kutokana na maneno yake ya utata kuhusu Conmebol baada ya mechi ya mshindi wa tatu kwenye mashindano ya Copa Amerika mwaka huu.