Back to top

Baba aliyekutwa mtupu na mwanae kwenye maporomoko kuchunguzwa akili.

21 December 2019
Share

Siku moja baada ya kusambaa mtandaoni kwa tukio la mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Benson Shila (31) akiwa kwenye  maporomoko ya maji ya mto Morogoro  eneo la mlimani Nguzo na mtoto wake  mdogo wa kiume wakiwa watupu majira ya jioni huku akiwa na panga na msumeno na kuzua hofu kwa wananchi jeshi la polisi mkoani Morogoro limesema  tayari limemtia mbaroni mtuhumiwa huyo na linaendelea na uchunguzi ikiwemo uchunguzi wa kiakili.

Kamanda polisi mkoa wa Morogoro SACP Wilbroad Mutafungwa amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa baada ya polisi kupata taarifa za raia wema  ambapo jitihada za askari zilifanikisha kumuokoa mtoto huyo.