Back to top

Kocha Simba atupa lawama TFF kuhusu uwanja.

29 August 2020
Share

Kocha wa Simba Sven Vandenbroeck ameilaumu TFF kwa kushindwa kusimamia maandalizi ya uwanja wa Shekh Amri Abeid Kaluta Arusha kwani hadi sasa bado eneo la kuchezea halijakamilika na timu kushindwa kufanya mazoezi kuelekea mchezo wao wa ngao ya jamii dhidi ya  Namungo. 

Na kuongeza kuwa hali kama hii ilijitokeza pia katika uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga katika mchezo wa fainali ya kombe la TFF "Azam Sports Federation Cup".

Kuelekea mchezo huo wa Ngao ya jamii kati ya Simba SC na Namungo FC Nahodha wa timu ya Simba John Rafael Boko amesema mchezo wa kesho ni muhimu kwao kuibuka na ushindi kwani ndiyo mchezo unaofungua msimu wa ligi hivyo wanataka kuanza vizuri.

Na upande wa Namungo FC Nahodha wa timu ya Namungo FC Hamisi Faki anasema wamejiandaa kupambana kuibuka na ushindi dhidi ya Simba kwani kikosi kipo tayari kwa mchezo huo huku kocha wa timu ya Namungo FC Thiery Hitimana amesema hawakuja Arusha kutembea wamekuja kupambana kwa nguvu zao zote kuhakikisha wanaifunga Simba na kutwaa Ngao ya Jamii.