Mashirika ya misaada yaliripoti watu wanne kukutwa na COVID-19 katika kambi ya Um Rakouba ya Sudan kwa wakimbizi wa Ethiopia wiki hii. Kambi hiyo ni makazi ya watu 25,000 ambao wamewasili tangu novemba mwaka jana
Wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu wiki hii wamethibitisha maambukizi hayo katika kambi za Sudan kwa wakimbizi waliokimbia mapigano katika mkoa wa Tigray nchini Ethiopia. Shirika la kuhudumia wakimbizi katika Umoja wa Mataifa-UNHCR na kundi la msaada la Mercy Corps wanasema uingiliaji wa haraka unahitajika ili kuepusha janga la kibinadamu.
VOA