Back to top

Rais Dkt.John Magufuli amefariki dunia akiwa na miaka 61.

18 March 2021
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John pombe Joseph Magufuli amefariki dunia, akiwa na umri wa miaka 61.

Taarifa rasmi ya kifo cha Rais imetangazwa kwa Umma na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mama Samia Suluhu Hassan usiku wa kuamkia leo kupitia Televisheni ya Taifa majira ya saa tano usiku Machi 17, 2021.

"Rais Magufuli amefariki kwa maradhi ya moyo katika Hospitali ya Mzena, alilazwa March 06,2021 katika Hospitali ya Jakaya Kikwete na kuruhusiwa March 7 na kuendelea na majukumu yake"

Makamu wa Rais Samia ameongeza kuwa "Machi 14 alijisikia vibaya na akarudi Hospitali ya Mzena, ambapo aliendelea na matibabu hadi umauti unamkuta"-Samia Suluhu - Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais Samia Suluhu ameeleza kuwa Rais Magufuli amekuwa akiugua tatizo la moyo kwa zaidi ya miaka 10

Makamu wa Rais amesema kuwa Nchi itakuwa na maombolezo ya siku 14 na bendera zitapepea nusu mlingoti.

                                     HISTORIA.
·1959- Azaliwa Chato kaskazini magharibi mwa Tanzania

·1995- Achaguliwa kuwa mbunge kwa mara ya kwanza

·2000- Ateuliwa kuwa Waziri

·2015- Achaguliwa kuwa rais kwa muhula wake wa kwanza

·2020- Achaguliwa kwa kipindi cha pili kuwa rais

·2020 Novemba 5 – Aapishwa kwa muhula wa Pili

·2021 Machi 6 - Alazwa katika taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete kwa tatizo la moyo la mfumo wa umeme

·2021 Machi 7 - Aliruhusiwa kurejea kazini

·2021 Machi 14 - Alikimbizwa Hospitali ya Mzena Dar es Salaam kuendelea na matibabu

·2021 Machi 17 saa kumi na mbili jioni - Magufuli afariki dunia.

https://www.youtube.com/watch?v=QFqrFSmfIIc