
Klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini iliyoitoa Simba robo Fainali ya Klabu bingwa barani Afrika imemfurumusha kocha wake Gavin Hunt.
Pamoja na kutinga Nusu Fainali Kocha huyo amekuwa akishutumiwa kwa kuwa na mchezo usiofurahisha huku Kaizer ikiwa nafasi mbaya tofauti ya alama 5 tu na timu ya pili kutoka mkiani Chippa United.
May 26 alipokea kichapo kutoka kwa Black Leopard na kuchochea kufungiwa virago tangu ajiunge na timu hiyo September 2020 na kuiongoza timu hiyo mechi 44 (ushindi 12,kupoteza 15 na sare 17) katika mashindano yote.