Back to top

Ajali ya basi la kampuni ya Classic yaua watatu Shinyanga.

02 June 2021
Share

Watu watatu wamefariki dunia na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa mkoani Shinyanga baada ya basi la kampuni ya Classic lililokuwa linatokea Kampala Uganda kwenda Jijini Dar es Salaam kuacha njia na kupinduka.

Mwandishi wetu Frank Mshana ametueleza kuwa abiria wengi waliokuwamo ndani ya basi hilo walikuwa ni wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Bugema kilichopo Kampala Uganda.