Back to top

Nusu fainali Yanga Vs Afc Leopards uwanja wa Uhuru.

08 June 2017
Share

Kikosi cha Yanga kikifanya mazoezi kwenye uwanja wa Uhuru Dar es Salaam ili kukwaana na AFC Leopards ya Kenya #SportPesaSuperCup

Hatua ya nusu fainali ya mashindano ya Sportpesa Super Cup 2017 yanafanyika hivi leo katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Mabingwa wa Tanzania Yanga watashuka dimbani kuvaana na Afc Leopards ya nchini Kenya huku Gormahia wakicheza na Nakuru All Stars.

Katika mechi ya leo timu itakayofanikiwa kumfunga mwenzake basi itakuwa imejikatia tiketi ya moja kwa moja kuingia katika fainali ya michuano ya Sportpesa Super Cup 2017 kuwania kitita cha Dola za kimarekani 30,000 sawa na Milioni 62 pesa ya kitanzania.

Timu ya Yanga ndiyo timu pekee inayoiwakilisha nchi ya Tanzania katika mashindano hayo baada ya Mabingwa wa Kombe la Shirikisho Simba SC, Singida United na Jang'ombe ya Zanzibar kutolewa mapema katika hatua ya robo fainali ya michuano yenye mvuto wa aina yake.