Back to top

“Tanzanite na Taifa Stars tembeeni Kifua mbele”. Waziri Bashungwa

27 August 2021
Share

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa l amezitembelea timu za taifa za wanawake (Twiga Stars na Tanzanite) katika viwanja vya  Kidongo chekundu maarufu kama JK Park jijini Dar es Salaam kujionea namna timu hiyo inavyoendelea na maandalizi kabla ya mchezo dhidi ya timu ya taifa ya wanawake ya Afrika Kusini mapema mwezi Septemba, 2021.

Akiwa katika viwanja hivyo Waziri Bashungwa ameongea na wachezaji wa timu hiyo akiwalezea adhima ya serikali katika kuinua michezo nchini na kuwapongeza wanamichezo wote kwa kuzidi kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kwa kuibuka vinara katika michezo mbalimbali.

Waziri Bashungwa amesema timu za wanawake za mpira wa miguu kwa maana ya Tanzanite na Twiga Stars zimebeba jina la Tanzania na taifa linajivunia kwa kuwa na timu hizo, ambazo mara kadhaa zimeweka historia ya kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali.

Kwa upande wake kocha wa timu za Taifa za wanawake Bakari Shime amemwelezea Waziri Bashungwa kuwa mashindano ya COSAFA yanayotarajiwa kufanyika nchini Afrika Kusini yatawasaidia kujiweka vizuri kwa ajili ya maandalizi ya kuwania kufuzu mashindano ya kombe la dunia mwaka 2022.