Back to top

Bei ya Korosho haina maslahi kwa mkulima Mtwara.

16 October 2021
Share

Wakulima wa Korosho wanaohudumiwa na Chama Kikuu cha Ushirika cha Masasi, Mtwara na Nanyumbu mkoani Mtwara wameuza korosho zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni kumi na saba katika mnada wa kwanza, wamepoteza matumaini ya kupata bei nzuri katika msimu wa mwaka huu 2021/2022.
.
Wakizungumza na ITV mwishoni mwa mnada wa Korosho katika kijiji cha Ruvango wilaya ya Masasi wamesema bei ya korosho katika msimu huu haina maslahi mazuri kwa mkulima.
.
Wameiomba serikali ikae na wanunuzi ili kujadili umuhimu wa kupandisha bei katika minada inayoendelea kwani kushuka kwa bei kunawakatisha tamaa.
.
Hata hivyo amesema zaidi ya tani elfu tano za korosho zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni kumi na saba na kuwaomba wakulima wasivunjike moyo kwa kupata bei hiyo kwani minada inayofuata bei itapanda.