Back to top

Kesi ya Mbowe yaahirishwa mpaka Oktoba 29, 2021.

28 October 2021
Share

Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imeahirishwa kesi ya uhujumu uchumi namba 16/2021 inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na wenzake watatu hadi kesho Oktoba 29, 2021.

Ni baada ya shahidi wa tatu wa upande wa mashtaka, ambaye alipaswa kuwepo mahakamani hapo kwa ajili ya kutoa ushahidi kushindwa kufika.

Wakili wa Serikali Mwandamizi Robert Kidando ameieleza Mahakama hiyo leo Oktoba 28, 2021, mbele ya Jaji Joachim Tiganga,  muda mfupi baada ya shahidi wa pili katika kesi hiyo Justine Kaaya kumaliza kuhojiwa .