
Wavuvi katika Kijiji cha Nyang’ombe wilaya ya Rorya Mkoani Mara wameiomba serikali kuangalia njia ya kutatua tatizo la kuvamiwa mara kwa mara na baadhi ya watu wanaodaiwa kutoka nchi za Kenya na Uganda na kuwanyang’anya mali zao pamoja na vifaa wanavyotumia kwaajili ya shughuli ya uvuvi.
.
Mkuu wa wilaya ya Rorya Mkoani humo Juma Chikoka amesema tayari taarifa za kuvamiwa kwa wavuvi hao zimefika katika ofisi yake na tayari anafanya mawasiliano baadhi ya viongozi katika nchi hizo waliopo katika ukanda wa ziwa ili kuangalia jinsi ya kutatua tatizo hilo.
