Back to top

DAKTARI AKAMATWA AKITOA MATIBABU NYUMBANI KWAKE.

30 October 2021
Share

Jeshi la Polisi wilaya ya Tandaimba mkoani Mtwara linamshikilia Daktari Karim Bakari kutoka kijiji cha Maheha kwa kosa la kutoa  huduma za matibabu kwa wagonjwa nyumbani kwake kinyume na taratibu na sheria inayosimamia sekta ya afya nchini.
.
Mkuu wa wilaya ya Tandaimba Kanali Patick Sawala ambaye ameongozana na kamati ya ulinzi na usalama wilaya imefanikiwa kubaini na kumkamata daktari huyo ambaye si mwajiriwa.
.
Amesema kukamatwa kwa daktari huyo kumetokana na uchunguzi uliofanywa kwa muda mrefu baada ya kupata taarifa hizo kutoka kwa wananchi na kulitaka jeshi la polisi wilayani humo kufatilia ni wapi alikuwa anapata dawa na vifaa tiba hivyo.
.
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Tandahimba Daktari Silas Sembiko amesema daktari huyo alifukuzwa kazi mwaka jana katika hospitali ya wilaya ya Newala kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji katika hospitali hiyo.
.
Hata hivyo amewataka wananchi kuacha tabia ya kupata huduma za afya vichochoroni kwa madai ni hatari kwa afya zao na kuwa tayari kutoa ushirikiano mara wanapobaini kuwapo kwa matibabu ya aina  hiyo.
.
Akijitetea daktari huyo amesema aliamua kufanya hivyo kutokana na msongo wa mawazo aliokuwa nao na kuomba serikali imsamehe.