
Bandari ya Mtwara imeanza kusafirisha makaa ya mawe yanayozalishwa hapa nchini kwenda nchini India ambapo mpaka sasa meli inayobeba bidhaa hiyo imepakia makaa ya mawe yenye uzito wa tani Elfu 33.
.
Mkuu wa mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Gaguti na kamati yake wametembelea bandari hiyo kujionea upakiaji wa makaa hayo ya mawe ukifanyika na kusema uwekezaji wa serikali katika ujenzi wa bandari hiyo uliyotumia zaidi ya shilingi bilioni 157 haujapotea bure.
.
Amesema meli hiyo itakuwa ikifanya safari zake nchini Tanzania kila mwezi
.
Kwa upande wake meneja wa bandari mkoa wa Mtwara Mhandisi Juma Kijavala amesema meli hiyo ya makaa ya mawe inaurefu wa mita 183 hivyo bandari inauwezo mkubwa katika kuhudumia meli kubwa.
