Back to top

MJEMA AONYA WANAOPANDISHA BEI VIFAA VYA UJENZI.

04 November 2021
Share

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi.Sophia Mjema ametoa onyo kwa wafanyabiashara ambao wameanza kupandisha bei za vifaa vya ujenzi ikiwemo  Saruji, Nondo na Mabati na kusababisha zoezi la ujenzi miradi ya fedha za UVIKO-19 zilizotolewa na Serikali kuanza kupata changamoto.
.
Mjema ametoa kauli hiyo wakati akikagua ujenzi wa mabweni na madarasa mawili katika shule ya sekondari Kishapu ambapo ameeleza kuwa baadhi ya wafanyabiashara wameanza kupandisha bei za vifaa vya ujenzi kinyume cha utaraibu na kumuagiza Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani humo kuanza kuwashughukikia wote wanaokiuka bei halali ya bidhaa hizo kwa makusudi.