Back to top

Maprofesa waongezewe muda wa kuwepo kazini.

06 November 2021
Share

Wakati Tanzania ikitajwa kuwa miongoni mwa nchi zenye uhaba wa wahadhiri wa vyuo vikuu, mamlaka husika zimeshauriwa kuangalia namna bora ya kuwaongezea muda wa kuwepo kazini maprofesa wanaofundisha vyuo hivyo  ambao hulazimika kustaafu kutokana na umri wao angali bado wanahitajika.

Ushauru huo umetolewa jijini Mwanza na Makamu Mkuu  wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine Balozi Profesa Costa  Mahalu wakati akizungumza na vyombo vya habari katika chuo hicho.

Aidha Balozi Mahalu amesema wanatekeleza maelekezo ya serikali ya kuwapokea wanafunzi wenye mkopo kutoka bOdi ya mikopo nchini  hata kabla ya fedha zao hazijaingia ili waweze kuendelea na masomo.

Nao baadhi ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza ambao wameshafika chuoni hapo  wamepongeza utaratibu huo utakaowagusa hadi watoto wanaotoka kwenye familia zenye kipato cha chini kupata elimu.