
Na Khalid Msabaha:
Kama ligi ingeanza mapema yani ingeanza mwezi Agosti tungepata timu ya Taifa yenye wachezaji weye Match fitness ya kutosha.
Msimu huu ligi ilianza Septemba 27, 2021 halafu mechi za kufuzu kombe la dunia zimeanza kabla ya ligi kuanza yani mechi za kufuzu kombe la dunia zilianza Septemba 02, 2021 kabla ya ligi kuanza, hapo wachezaji wanakuja timu ya taifa huku fitness zao haziwezi kulingana na wale wanaotoka nchi ambazo ligi zimeanza mwezi wa Augosti yani wanajiunga timu zao za taifa wakiwa wamepata mechi nyingi hivyo wanakuwa bora kuliko sisi.
.
Ndio maana sikushangaa Stars kufungwa na Benin hapa Dar, na Jana kufungwa tena goli 3-0 dhidi ya DR Congo, maana yake tungekuwa tumeshinda dhidi ya Benin hapa tungekuwa tunaendelea kubishana na DR Congo hadi sasa kuwania hatua ya tatu kufuzu kombe la dunia 2022 Qatar.
.
DR Congo wachezaji wao kama akina Arthur Masuako na wengineo wametoka Ulaya ambapo wamepata Pre season nzuri halafu wamecheza mechi nyingi ndio maana wenzetu walikuwa bora kuliko sisi.
.
Ndio maana hata kocha wa DR Congo hakumtumia Djuma Shaban wa Yanga kwani hata yeye akiwa Yanga alicheza mechi ngapi kwenye ligi kuu bara?
.
Angalia timu zetu za ligi kuu yani hazikuwa na Pre Season nzuri kabla ya ligi kuu kuanza, kwani ligi msimu uliopita ilichelewa kuisha yani ligi ilifika July muda ambao wachezaji walipaswa kuwa wameshapumzika na wanarejea kambini kujiwinda na msimu mpya ambao ulipaswa kuanza mwezi Agosti.
.
Matokeo yake msimu huu ligi imeanza timu zinacheza mechi mbili wachezaji wanarudi timu ya taifa zinacheza mechi mbili wanarudi tena ligi kuu, wanacheza mechi mbili wanarudi tena timu ya taifa.
.
Kwa kawaida huwezi pata mchezaji mwenye Match fitness ya kutosha kwenye timu ya taifa kwa sababu ubora wa mchezaji wa timu ya taifa unatokana mechi nyingi alizocheza kwenye ligi na timu yake.
.
Hivyo ningependa kuona bodi ya ligi TPLB hawarudii makosa wanajifunza kupitia hili na kuepusha ligi kuchelewa kuisha na kuchelewa kuanza msimu mpya ili kuwapa muda wa kutosha wachezaji kupumzika na muda wa kutosha kurejea kambini kupata Pre Season na vilabu vyao.
#NiMtazamoTu
