
Watu wawili wamekufa na wengine ambao idadi yao haijajulikana wamejeruhiwa kufuatia milipuko miwili ya mabomu kutokea katikati ya mji wa Kampala nchini Uganda.
.
Kwa mujibu wa mashuhuda milipuko hiyo imetokea karibu na ofisi za bunge na karibu na baadhi ya wizara muhimu za Serikali ya nchi hiyo.

Kutokana na milipuko hiyo vyombo vyote vya usalama nchini humo vimeimarisha ulinzi katika maeneo hayo na hakuna mtu ambaye anaruhusiwa kuingia ama kutoka maeneo husika.
.
Mpaka idara za usalama nchini humo hazijatoa taarifa za kina kuhusiana na milipuko hiyo.
