
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Mauritius mwenye makazi yake Harare, Zimbabwe, Prof. Emmanuel Mbennah amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu Rais wa Jamhuri ya Mauritius Mhe.Eddy Boissezon, GOSK.

Katika mazungumzo hayo viongozi hao wameonesha utashi kuona kwamba ushirikiano baina ya Nchi hizo unazidi kuimarika katika nyanja za uchumi, biashara utalii na uwekezaji.
.
Makamu wa Rais pia ameipongeza Tanzania kwa Mtanzania Abdulrazak Gurnah kushinda Tuzo ya Amani ya Fasihi.
