Back to top

TARURA YAPEWA RUNGU KUWABANA WAKANDARASI.

19 November 2021
Share

Serikali ya Mkoa wa Mtwara imeuagiza Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA) kuwachukulia hatua kali baadhi ya wakandarasi watakaokiuka mikataba ya ujenzi wa barabara zinazojengwa kwa kiwango cha changarawe katika halmashauri sita na kugharimu shilingi Bilioni tatu nukta sita.
.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara  Brigedia Jenerali Marco Gagutiwakati akishuhudia wakandarasi kumi wakitia saini mikataba ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha changarawe katika halmashauri sita za Mkoa wa Mtwara.
.
Amewataka wakandarasi hao kuzingatia mikataba waliotia saini ikiwa ni pamoja na kuzingatia ubora wa kazi lakini muda uliyopangwa ili kukabidhi kazi hiyo kwa wakati.