Back to top

Watatu wafariki kwa kula samaki aina ya kasa.

27 November 2021
Share

 

Watu watatu wamefariki dunia na wengine ishirini na wawili wamelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Micheweni kisiwani Pemba baada ya kula samaki aina ya kasa. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kaskazini Juma Sadi amesema wagonjwa waliolazwa hospitali ya Micheweni wanaendelea vizuri, huku akibainisha kuwa matukio kama hayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara katika maeneo hayo, licha ya wataalam kukataza samaki huyo asiliwe kutokana na sumu aliyo nayo.