
Boti ya kwanza kutoka bandari ya Libya ya Misrata Jumatano imeng’oa nanga kuelekea kwenye mji wa bandari wa Izmir, Uturuki, ikiwa ni miaka 40 tangu safari ya mwisho kama hiyo kufanyika.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, Libya haijapata huduma za boti za kimataifa kwa takriban miaka 25.
Safari za baharini pamoja na zile za ndani nchini humo zilisimama kuanzia mwaka 2011 baada ya mapinduzi yaliyomuondoa kiongozi wa muda mrefu Muammar Gaddafi.
Safari boti ambazo chukua saa 48 kufika Uturuki zimefufuliwa tena na kampuni ya Libya ya Kavalay, ambapo boti hiyo ya kwanza inatarajiwa kurejea Libya Desemba 7.
#VOA
