
Mtu moja raia wa Msumbiji, aliyejulikana kwa jina la Simon Faducane amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela na kulipa faini ya shilingi bilioni moja na milioni tisini na sita huku gari lake likitaifishwa na serikali baada ya kukutwa na hatia ya kusafirisha kilo nane za dawa za kulevya aina ya heroin.
.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa na jeshi la polisi akiwa na dawa hizo za kulevya akiziingiza nchini kupitia mpaka wa Kasumulu wilayani Kyela na kupelekwa moja kwa moja mahakamani ambako amekiri kosa lake.
