Back to top

Wanaomiliki silaha kinyume cha sheria kusakwa

06 December 2021
Share

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.George Simbachawene ameliagiza Jeshi la Polisi nchini  kufanya msako mkali wa kuwabaini watu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria, Mhe. Simbachawene ametoa agizo hilo kufuatia kumalizika kwa muda wa kusalimisha silaha hizo huku akibainisha kuwa asilimia kubwa ya silaha zilizosalimishwa ni silaha za kienyeji hususani magobore.