Back to top

Tahadhari Uviko-19 Mbezi Luis, Gwajima asikitishwa.

06 December 2021
Share

Waziri wa Afya, Dkt.Dorothy Gwajima amesikitishwa na uzembe wa watendaji kushindwa kufuata maelekezo na miongozo ya Wizara ya Afya ya kuchukua tahadhari juu ya Ugonjwa wa Uviko-19 kwa kuweka vitakasa mikono, maji tiririka na kuhimiza wananchi kunawa mikono na kuvaa barakoa kabla ya kupanda gari katika Kituo Kikuu cha Mabasi ya Abiria cha Magufuli.
.
Waziri Gwajima ametoa kauli hiyo baada kufanya ziara ya kushtukiza katika kituo kikuu cha mabasi cha Magufuli kilichopo Mbezi Luis Jijini Dar es salaam kinachotoa huduma kwa wananchi zaidi ya 12,000 kwa siku huku vifaa vya kunawa mikono vikiwa havitoshelezi.