
Serikali imetoa wito kwa Asasi za Kirai nchini kuendelea kushirikiana na Serikali katika maeneo mbalimbali ili kuchochea maendeleo ya pamoja kwa kuwa nchi inahitaji mawazo ya pamoja ili kusukuma gurudumu la maendeleo kwa manufaa ya Wananchi na Taifa kwa ujumla.
Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mhandisi Hamad Masauni wakati wa Uzinduzi wa Tamasha la Kitakwimu la Mwaka 2021 (Data Tamasha 2021) kuhusu matumizi ya takwimu kwenye uchumi wa kidijitali lililofanyika jijini Dar es salaam.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Mifumo ya Fedha, Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. John Sausi, alisema kuwa Serikali chini ya wizara mwaka 2017 ilianzisha Mpango Mkakati wa Uchumi wa Kidijitali.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya dLab, Bw. Sosthenes Sambua alisema wataendelea kushirikiana na Serikali ili kuhakikisha malengo ya Taifa yanafikiwa kwa wakati.
