Back to top

Mwili wa mfanyabiashara aliyeuawa wasafirishwa.

08 December 2021
Share

Mwili wa Mfanyabiashara wa vitunguu Jackson Charles  aliyeripotiwa kupotea tangu Oktoba 22 mwaka huu huko wilayani Wangingombe mkoani Njombe umekutwa katika msitu wa Ngaramaro kijiji cha  Mtapa wilayani humo  na kusafirishwa kwenda kuzikwa kwao wilayani Kilosa mkoani Morogoro.

Kwa mujibu wa uongozi wa Kata ya Kidugala wilayani Wangingombe ambako marehemu alikuwa anafanyia biashara  mwili wa mfanyabiashara ulikutwa katika msitu huo ukiwa umeharibika na baaadhi ya viungo vikiwa havipo na serikali ikachukua jukumu la kuuzika hapo Desemba 5 mwaka huu.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe Hamis Issa amethibitisha kushikiliwa kwa mtuhumiwa mmoja kutokana na tukio hilo.