Back to top

Watendaji simamieni maelekezo ya viongozi.

09 December 2021
Share

Waziri wa Afya, Dk. Dorothy Gwajima amewaagiza watendaji kusimamia maelekezo ya viongozi wa ngazi za juu na kuyafanyia kazi kwa wakati ili kutoa mrejesho wa utekelezaji kwa wakati kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wenye tija kwa manufaa ya Taifa.
.
Waziri Gwajima ametoa wito huo wakati akifungua kikao kazi cha kuwasilisha utekelezaji wa maazimio ya Mkutano Mkuu wa Chama cha Wafamasia Tanzania kilichofanyika Mwezi Mei jijini Dar es salaam.