Back to top

Muliro atoa tamko mechi ya Watani wa Jadi.

10 December 2021
Share

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam limesema limejipanga kuhakikisha ulinzi unaimarishwa katika mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga Disemba 11, 2021 utakaochezwa majira ya saa kumi na moja jioni katika uwanja wa Benjamini Mkapa lengo ni kuwafanya mashabiki wa mpira wa miguu watakaoshuhudia mchezo huo kuwa  kwenye mazingira ya amani na utulivu.


Pia Jeshi la Polisi  limepiga marufuku kwa mtu yeyote asiyehusika na mambo ya kiusalama kuingia uwanjani na silaha yoyote ikiwemo silaha za moto, visu, Panga au mawe .