Back to top

Serikali kujenga majosho 178 mwaka wa fedha 2021/22

12 December 2021
Share

Wizara ya Mifugo na Uvuvi, imesema katika mwaka wa fedha 2021/2022 imepanga kujenga majosho ya kuogeshea ng'ombe 178 ili kuiepusha mifugo na magonjwa yanayosababishwa na Kupe na maradhi mengine yanayoambatana na kutokuogesha mifugo. 
.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki alipokuwa katika ziara ya kukagua miundombinu ya majosho iliyopo wilayani Bunda, mkoani Mara.