Back to top

Hata kama hawezi kunyanyuka nitaishi nae.

14 December 2021
Share

Mwanamke mmoja mkazi wa Benue nchini Nigeria amewaacha wengi vinywa wazi baada ya kuamua kufunga pingu za maisha na mpenzi wake wa miaka 27 Terkimbir Benjamin Tyough mwenye umri wa miaka 45 ambaye hawezi kutoka kitandani baada ya kupata ajali.

Bw Terkimbir  ni fundi wa umeme na alivunjika uti wa mgongo baada ya kuanguka kutoka kwenye mnara wa umeme mwezi Machi mwaka 2021.


Mke wa Terkimbir Bi Christiana baada ya picha za harusi yao kusambaa kwenye mitandoa ya kijamii amesema hata kama mume wake hawezi kunyanyuka kitandani ataishi naye maisha yake yote yaliyobaki kwa kuwa mapenzi aliyonayo kwa mume wake sio madogo na ndoa yao itadumu daima