Back to top

Corona: Wanasayansi wa Urusi wawasili S.Africa.

14 December 2021
Share

Kundi la wanasayansi wa Urusi limewasili nchini Afrika Kusini kuchunguza aina mpya ya Kirusi cha Corona(Omicron) iliyogundulika kwa mara ya kwanza nchini humo. Wizara ya mambo ya nje ya Urusi imetoa taarifa hizo kupitia mtandao wake wa Twitter ambapo iliongeza kuwa ndege hiyo imebeba maabara inayotembea itakayotumika katika uchunguzi wa kirusi hicho.