Back to top

Omicron: Kenya Yaripoti wagonjwa watatu wa kwanza.

15 December 2021
Share

Maafisa wa afya nchini Kenya wamethibitisha wagonjwa watatu wa kwanza wa aina mpya ya kirusi cha corona kijulikanacho kama Omicron. Akizungumza wakati wa mkutano wa mashauriano na Baraza la Magavana kujadili sera ya afya na vikwazo vya kisheria, Waziri wa Afya nchini humo Mutahi Kagwe alithibitisha kuwa aina hiyo mpya ya virusi hivyo imegunduliwa kwa abiria watatu ambao tayari wamewekwa karantini.